Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) –ABNA– Waziri wa Sayansi, Utafiti na Teknolojia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hussein Simayi, amewasilisha mapendekezo matatu ya kiutendaji yenye lengo la kupanua ushirikiano wa vyuo vikuu, utafiti na teknolojia kati ya nchi wanachama wa Shirika la Ushirikiano wa Shanghai.
Simayi alitoa mapendekezo hayo aliposhiriki katika mkutano wa wakuu wa vyuo vikuu vya nchi za Shirika la Ushirikiano wa Shanghai uliofanyika mjini Minsk, Belarus, ambapo alisisitiza umuhimu wa kubadilisha ushirikiano wa kisayansi kuwa miradi ya utekelezaji wa moja kwa moja.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRNA, Waziri Simayi alisema katika hotuba yake kuwa vyuo vikuu ni nguzo kuu katika kujenga mustakabali wa jamii na maendeleo ya mataifa.
Ameongeza kuwa ushirikiano wa kielimu na kiutafiti kati ya nchi wanachama unapaswa kuimarishwa zaidi ili kuleta matokeo ya vitendo yanayochangia maendeleo ya teknolojia na ustawi wa pamoja.
Your Comment